Wanafunzi Wavamiwa na Kunguni katika Chuo Kikuu cha Pwani

0
Pwani University

By Isaac Nyaribari.

Tangu kusajiliwa rasmi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Pwani hapo Julai tarehe mbili moja kwa moja baadhi ya wanafunzi waliotafuta makazi ndani ya shule walikabidhiwa vyumba vyao rasmi hasaa wale wachache waliobahatika kupata nafasi hiyo. Lakini tangia Julai ishirini baada ya wanafunzi hao kumaliza majuma mawili hivi hali ikawa si hali tena katika vyumba mbalimbali vya kulala kwani mdudu kunguni alianza kupiga kambi ndani ya baadhi ya vyumba vya wanafunzi hao japo sio vyote.

Hali ikabadilika sasa sio kulala kwa giza tena ni kulala kwa mwangaza taa zikiwa zimewaka ili angalau kuona kama makali ya mdudu kunguni yanapungua kwani walikuwa wameteka anga kwenye vyumba hivyo kwa takribani asilimia sabini ya vyumba hivyo. Baadhi ya vyumba vilivyoathirika ni kama: chumba nambari moja na chumba nambari mbili ambavyo ni vya wanaume vilevile chumba
nambari tatu ambacho ni cha kina dada. Hata hivyo chumba nambari sita maarufu kama Runda hakikuathiriwa na jaramanda hilo kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na vyumba vingine.

Baada ya athari hizo kuenea, ikawa sasa jua chomoza godoro anika kunguni fukuza. Ungeona pindi tu jua lichomozapo wanafunzi chuoni wanayatandika malazi yao juani ili kupigwa na miale ya jua kuona kana kwamba wanapunguza makali n ya kunguni yaliyokuwa yamekithiiri vilevile kuwafukuza adui wa usingizi waliokuwa wamepewa jina la utani kama “watchman” kumaanisha mlinzi wa usiku ikizingatiwa kwamba kunguni walikuwa wakiwafanya wanafunzi kukosa usingizi.

Lakini hali hii ya kunguni kukithiri kwenye chuo kikuu cha Pwani haikuwa ya kawaida kwani kulingana na wanafunzi nioliosema nao kuhusiana na swala zima kunguni Pwani wanasema kwamba likizo ya viongozi wa wanafunzi ilichangia masaibu yao kwa kiasi Fulani kwani viongozi hao ndio huwa na sauti ya kusikika na hata usimamizi wa chuo hicho. Hivyo basi kumaanisha kwamba
wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikosa mtetezi wakati wa swala lenye uzito kama hilo.

Kadri muda ulivyoendelea kusonga ndivyo usimamizi wa chuo kikuu cha Pwani ulikuja kugundua kwamba kunguni kukithiri kwenye vyumba vya wanafunzi lilikuwa donda sugu ndiposa wakachukua hatua za haraka kwa kununua dawa ambazo zilitumika katika kusafisha vyumba na kuwafukuza kunguni hao kutoka kwa vyumba vya wanafunzi na kupunguza makali ya kunguni hao.

Hata baada ya kufanya shughuli nzima ya kuyaosha malazi ya wanafunzi kutumia dawa kuwaua kunguni bado hali ni tete chuoni Pwani kwani kwa asilimiia takribani arubaini hivi kunguni bado wapo kwenye baadhi ya vyumba vya kulala vya wanafunzi hao ambacho vilevile ni kinaya kwa wanafunzi hao ambao walikuwa na taswira ya kuvutia wakija chuoni ili kutimiza ndoto zao za maisha.Lakini sasa yale mazingira ambamo wamo kwa hivi sasa hayalingani na yale mawazo ambayo walikuwa nayo hapo awali.

Kwa hivi sasa wanafunzi hao wanaomba usimamizi wa chuo hicho kufanya hima ili kuona kwamba makazi ya wanafunzi yananadhifishwa ili yawe katika hali nzuri inayotia moyo.

Lakini baadhi ya wanafunzi hao washapoteza imani na makazi ya chuo hicho na wana mpango kuyahama hapo mwanzoni mwa mwaka na muhula mpya ili kujitafutia makaziu nje ya chuo hicho ambvayo yamo katika hali nzuri.

Comments

comments

Comrade, Share your Thoughts Here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.